UJUMBE UNAOWEZA KUBADILISHA MAISHA
MAANDIKO: 1KOR 9: 24 - 25
TAR 06.08.2017
TAR 06.08.2017
Katika maisha ya mwanadamu kuna jumbe mbalimbali ambazo zinaweza kubadilisha maisha. Kuna mtu anaweza kupokea ujumbe kutoka kwa mzazi, ndugu, rafiki, jamaa au mtu yeyote ambaye yupo karibu nawe na ujumbe huo ukakubadilisha maisha yako. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kudumu au muda tu. Tena ujumbe huo unaweza pia usiwe wenye faraja kwako.
Lakini upo ujumbe ambao unaweza kuleta mabadiliko katika maisha yako na yakaleta furaha ya milele. Ujumbe huo ni Neno la Mungu. Biblia ndiyo iliyobeba ujumbe huo wa Neno la Mungu. Biblia ina majibu ya maswali yako. Isome mpendwa.
Katika Neno kuna faida nyingi kati ya hizo ni:-
- Inatoa njia ya kwenda mbinguni.
- Huleta amani ya kweli ndani ya moyo (Yoh 14:17)
- Huponya magonjwa
- Hukaa moyoni mwa mtu
- Neno linaishi milele.
- Huona kilichopo moyoni mwa mtu
Mpenda dumu katika Neno la Mungu ili uwe na badiliko la kweli moyoni mwako. Mapito yako yasikufanye uache kuliishi katika Neno. Petro alimwambia Yesu kwa neno lako nitashusha nyavu. Liamini Neno.
Maandiko mengine
Math 7:24 - 27, Yoshua 1:8, na 1Tim 4:15
MHUBIRI
SAMWEL ZAYUMBA
KUTOKA TAG MWENGE - DSM
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni