SAA YA TAABU YAKO INAPITA
2WAFALME 4: 1 -7
Tarehe 21.05.2017
Saa ya taabu inapofika huumiza, huteta majuto, huteta maswali mengi, huleta manung`uniko, huwa na uchungu, hukosesha amani moyoni, huondoa furaha nakadhalika. Kwa upande wa mtu wa Mungu saa ya taabu inapofika huweza kumwondoa katika uwepo wa Mungu.
Mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha kwa habari za watoto wake wawili kutaka kuchukuliwa ili wawe watumwa. Huyu mama alifiwa na mmewe na hakuwa na mali nyingi za kukidhi haja maisha yake ya kila siku. Yumkini alikuwa na madeni mengi hata yakampelekea kushindwa kulipa. Hakika ilikuwa saa ya taabu yake. Lakini Mtumishi wa Mungu Elisha alipofika nyumbani kule mama, mama yule akamwambia habari za watoto wake kutaka kuchukuliwa kuwa watumwa. Elisha akamwambia wataka nikufanyie nini? Niambie una kitu gani nyumbani? Mama yule akajibu akasema mimi ni mjakazi wakosina kitu nyumbani ila chupa ya mafuta. Ndipo Elisha akamwambia akisema nenda ukatake vyombo huko nje kwa majirani zako wote vyombo vitupu wala usitake vichache. Kisha uingie ndani ukajifungie mlango wewe na wanao ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote. Mama yule akafanya hivyo ndipo vyombo vyote vikajaa mafuta. Biblia inatuambia vyombo vilipokuwa vimejaa Mtumishi Elisha akamwambia mama niletee tena chombo. Mama akajibu akisema hakuna tena chombo. Hivyo mama yule saa ya taabu yake ikawa mwisho kwani mafuta yale aliyauza na kulipa manedi ili watoto wake waliende utumwani
Ndugu saa ya taabu yako inapita tu. Kwa nini kufadhaika, kuhangaika na hata kuvunjika moyo kwa taabu yako unayoipita. Kumbuka saa ya taabu inapita tu. Yesu yupo alipigwa msalabani kwa ajili ya taabu yako. Usimwache Yesu kwa taabu yayo unayoipitia. Ayubu hakumwach aMungu kwa taabu yake aliyoipata. Mweleze Yesu taabu yako naye atakutokea. SAA YA TAABU INAPITA USIOOGOPE.
Mhubiri
Mchungaji. Mary Mneo