Jumapili, 21 Mei 2017

YESU NDIYE SULUHISHO LAKO

UJumbe: YESU NDIYE SULUHISHO LAKO
Maandiko: Luka 5:12 - 14
Tarehe 30.04.2017

Ukoma katika jamii ya Israel ilikuwa ni tatizo kubwa mno. Mtu mwenye ukoma ililazimika kutengwa  kama tunavyosoma maandiko Mambo ya Walawi 13 - 14.

Hata sasa dunia huwatenga watu wenye ukoma. Ukoma hushambulia mwili na hata mfumo wa fahamu. Kwa zama za Agano la Kale mtu mwenye ukoma alitengwa kwa muda fulani mpaka atakapotasika na baada ya kutakaswa atoe sadaka maalumu. Kuhani alihusika kumkagua mtu mwenye ukoma kama ametakasika au la. Mtu mwenye ukoma akichangamana na watu wasio na ukoma sheria iliwaruhusu kumwua mtu huyo kwa mawe. 

Siku moja mwenye ukoma alisikia habari za Yesu na akazimia moyoni mwake kwenda kwake ili aponywe na ukoma. Ugonjwa huo ulimtesa kwa siku nyingi akaanguka kifudifudi mbele za Yesu akisema " Bwana ukitaka waweza kunitakasa". Ndipo Yesu akaunyoosha mkono wake akisema nataka takasika. Mara mtu mwenye ukoma wake ukamwondokea. 

Imani ya mtu mwenye ukoma ilimfanya atakasike na akawa huru kuchangamana na watu wengine

Mtu wa Mungu ukoma ni dhambi ambayo hutufanya tufarakane na Mungu. Ni kitu gani kwako ambacho ni ukoma kinakufanya usipokee muujiza wako? Nenda mbele za Bwana umweleze mambo yako na akurehemu ndipo upokee haja ya moyto wako kama vile mtu yule aliyekuwa na ukoma alipomwendea Yesu na kuanguka kifudifudi.


Mhubiri
Mchungaji Jonas Charles Shebila
T.A.G Michungwani Muheza



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni