Jumapili, 23 Aprili 2017

UMEJIANDAEJE KWA AJILI YA UNYAKUO

Mchungaji Kiongozi akitoa ujumbe

IBAADA YA TAREHE 23.04.2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI KIONGOZI PASCAL MNEO
MAANDIKO: Math 24: 15 - 26
UJUMBE: Umejiandaaje kwa ajili ya unyakuo.

Utangulizi:
Wanafunzi wa Yesu walitaka kufahamu mambo matatu kutoka kwa Yesu ambayo ni 
  1. Tuambie lini yatatukia hayo
  1. Dalili ya kuja kwako (Yesu Kristo)
  1. Mwisho wa dunia itakuwa lini
Ujumbe huu ni mwendelezo wa jumbe zilizopita kama majuma mawili yaliyopita. Yesu aliwajibu wanafunzi wake kama tunavyoma kwenye Injili ya Mathayo 24:15 " Hapo mtakaliona chukizo la uharibifu lile lililonenwa na Nabii Daniel limesimama katika patakatifu(asomaye na afahamu)"
Wakati ukifika kutakuwa na dhiki kubwa, ambayo haijawahi kutokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa wala haitakuwapo tena. Chukizo la uharibifu (mpinga kristo) atakapoingia hekaluni atafanya mambo makuu, pia watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza kama yamkini hata wateule. Mateso na dhiki kuu itatokea nani atastahimili mateso hayo? Tiketi yetu ni kujiandaa kwa ajili ya unyakuo. Asitokee mtu awaye yeyote kukunyang`anya taji yako. Angalia njia za maisha yako. Wokovu wako uwe thabiti mbele za Mungu.
Hakikisha unajiandaa vyema kwa ajili ya unyakuo ili usije kupata mateso hayo ambayo Yesu anasema itakuwa kilio na kusaga meno.

Mwisho.

Kanisa likizidi kuongeza baada ya mama mmoja kukubali kuyakabidhi maisha yake kwa Yesu

 
Wachungaji wakifanya maombozi maalumu kwa washirika waliohitaji maombi.
 










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni