IBAADA YA TAREHE 02.04.2017
MAANDIKO: Math 24: 36 - 44
Mhubiri: Mchungaji
Ujumbe: Kunyakuliwa kwa kanisa
Mathayo aliitwa na Bwana Yesu na kuambiwa "nifuate". Mathayo alimfuata Yesu bila ya kujiulizauliza. Hivyo Mathayo akawa miongoni mwa wale Thenashara ( wanafunzi 12).
Yesu alianza kueleza namna siku hiyo itakavyokuwa kwa kuanza na mfano wa Gharika wakati wa mtumishi wa Mungu Nuhu. Watu waliendelea kufanya shughuli zao na Nuhu hakuacha kuwaambia watu habari za mpango wa Mungu wa kugharikisha ulimwengu. Nuhu aliwaitwa watu waje watengeneze safina ili waokolewe lakini watu hawakujali na walimwona Nuhu kama mtu aliyechanganyikiwa. Kwenye gharika hiyo alipona Nuhu na familia yake tu.
Ndipo hata siku ya unyakuo itakapokuja watu watakuwa wakiendelea kufanya shughuli zao za kila siku. Parapanda itakapolia watakaosikia ni wale walioishi maisha matakatifu. Hao ndio watakaonyakuliwa.
Mpendwa umejiandaaje kwa ajili ya unyakuo? Mpendwa endelea kuishi maisha matakatifu. Kufumba na kufumbua Yesu atakuja kulichukua kanisa lake. Itakuwa ni kilio cha kusaga meno kwa mtu ambaye hatatwaliwa siku hiyo. Ni wakati wako sasa kuyanagalia maisha yako kama yanamlingana Mungu ili uwe miongoni mwa wale watakao nyakuliwa siku hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni