IBADA YA TAREHE 19.03.2017
MHUBIRI: NDG DICKSON A. MFIKWA
UJUMBE: Nanyi mwaninena kuwa mimi ni nani?
Maandiko: Math 16: 13 - 16
Utangulizi
Kitabu cha kwanza kabisa katika Agano Jipya ni kitabu cha Injili ya Mathayo. Kitabu hiki kinasadikiwa kiliandikwa na Mathayo Mwenyewe kwenye mwaka 65 - 70 BK. Lengo la kuandikwa kwa kitabu hiki ilikuwa kuthibitisha kuwa Yesu Kristo ni Masihi wao wa kweli.
Somo lenyewe.
Maana ya Masihi au Masiya:
Mtu anayeaminiwa na wakristo kuwa ni Mwana wa Mungu aliyezaliwa kuwaokoa watu dhidi ya dhambi, Mkombozi, Yesu Kristo (kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu).
Siku moja Yesu akaamua kuwauliza wanafunzi wake kuhusu maisha yake akitaka kufahamu hasa watu wanamnenaje kuhusu yeye mwenyewe. Kwa maana nyingine aliamua kufanya tathmini ya maisha yake. Kupitia maisha au huduma ya Yesu Kristo aliyokuwa akifanya watu walimnena kuwa yeye huhenda ni Yohana Mbatizaji, Elia, Yeremia au miongoni mwa Manabii. Hivyo ndivyo wanafunzi walivyojibu swali ambalo Yesu Kristo alilouliza. Yesu hakuishia hapo akawauliza tena wanafunzi nanyi mwaninena kama mimi ni nani? Ndipo Petro akajibu kuwa wewe ni Mwana wa Mungu aliye hai.
Zipo sababu zizowafanya watu wengine waseme kuwa Yesu Kristo ni Yohana Mbatizaji, Elia, Yeremia au ni miongoni mwa Manabii. Kati ya sababu hizo ni nguvu alizokuwa nazo Yesu Kristo katika huduma yake kama vile vipofu waliona, viwete walitembea, wenye ukoma walitakasika, wafu walifufuka, wenye mapepo walitolewa, wagonjwa walipata nguvu nakadhalika.
Maisha mkristo wa leo
Nasi katika maisha tunayoyaishi hatuna budi kujifanyia tathmini kama Bwana wetu Yesu Kristo alipoamua kujitathmini juu ya maisha yake kwa watu waliokuwa wakimzunguka pamoja na wanafunzi wake. Leo maisha yetu yamezuia nguvu za Mungu kutendeka ndani ya kanisa kwa sababu ya ushuhuda wa maisha yetu kwa watu waliopo ndani na nje ya kanisa. Inatupasa kufanya tathmini ya maisha yetu ili tuweze kubalika na kumlingana Bwana wetu Yesu Kristo. Tuone ni wapi tunakosea na kutubu kama Isaya alivyofanya (Isaya 6:5). Matendo, Maneno na mawazo yawe safi mbele za Mungu.
Madhara ya kutenda dhambi
- Utasababisha hata asiye na hatia kuangamia kwa ajili yako. (Yoshua 7: 1, 5, 20, 24)
- Nguvu za Mungu hazitendi kazi ndani yetu
Hitimisho.
Mpendwa tukitaka nguvu za Mungu zitende kazi ndani yetu na watu wengine waokolewe hatuna budi kuacha kutenda dhambi na kuishi maisha yenye ushuhuda mzuri mbele za Mungu.