IBAADA YA TAREHE 26.3.217
MHUBIRI: Ndg VERONICA MALUWA
UJUMBE: Je umeimimina roho yako kwa nani?
Maandiko: 1Samwel 1: 9 - 20
1Samwel 1:15 ( ......... mimi sikunywa divai wala kileo ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana).
Utangulizi:
Kumimina roho kwa Bwana ni ile hali ya kupeleka au kueleza haja ya moyo kwa Mungu kwa unyenyekevu mkuu.
Palikuwa na mtu mmoja mcha Mungu aliyeitwa Elkana. Naye Elkana alikuwa na wake wawili mmoja aliitwa Hana na wa pili aliitwa Penina. Penina alikuwa na watoto lakini Hana hakuwa na mtoto kwa wakati ule kwa Mungu alimfunga tumbo lake kwa muda. Moyo wa Hana ulikuwa na huzuni kwa kukosa mtoto ndipo akaamua moyoni mwake kuimimimna roho yake kwa Bwana. Mungu akasikia haja ya moyo wake hatimaye akapata mtoto wa kiume akamwita jina Samwel.
Ujumbe
Katika maisha yetu ya kila siku yapo mahitaji mbalimbali na mengine ni magumu kwetu lakini ukiimimina roho yako kwa Bwana naye atafanya kwa ajili yako. Yeye ni mwaminifu ukitembelea pamoja naye kama Hana alivyofanya.
Faida ya kuimimina roho yako kwa Bwana
- Bwana atakulinda (Mdo 16: 25)
- Bwana atakuinua (Mwanzo 41: 45)
- Kwake yeye ni kimbilio na nguvu (Zab 46:1)
Hitimisho
Inawezekana mpendwa hupokei haja ya moyo wako kwa kuwa hujaimimina roho yako kwa Bwana. Mimina haja ya moyo wako kwa Bwana naye atakutokea. Kwa Mungu wetu hakuna jambo asiloliweza tazama mfano wa Shadrack, Meshack na Abedinego katika tanuri la moto Mungu alichowafanyia. Tusikate tamaa wala kumtenda Mungu dhambi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni