Jumapili, 6 Agosti 2017

UJUMBE UNAOWEZA KUBADILISHA MAISHA

UJUMBE UNAOWEZA KUBADILISHA MAISHA 
MAANDIKO:  1KOR 9: 24 - 25
TAR 06.08.2017

Katika maisha ya mwanadamu kuna jumbe mbalimbali ambazo zinaweza kubadilisha maisha. Kuna mtu anaweza kupokea ujumbe kutoka kwa mzazi, ndugu, rafiki, jamaa au mtu yeyote ambaye yupo karibu nawe na ujumbe huo ukakubadilisha maisha yako. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kudumu au muda tu. Tena ujumbe huo unaweza pia usiwe wenye faraja kwako.

Lakini upo ujumbe ambao unaweza kuleta mabadiliko katika maisha yako na yakaleta furaha ya milele. Ujumbe huo ni Neno la Mungu. Biblia ndiyo iliyobeba ujumbe huo wa Neno la Mungu. Biblia ina majibu ya maswali yako. Isome mpendwa.

Katika Neno kuna faida nyingi kati ya hizo ni:-

  1. Inatoa njia ya kwenda mbinguni.
  2. Huleta amani ya kweli ndani ya moyo (Yoh 14:17)
  3. Huponya magonjwa
  4. Hukaa moyoni mwa mtu
  5. Neno linaishi milele.
  6. Huona kilichopo moyoni mwa mtu
Mpenda dumu katika Neno la Mungu ili uwe na badiliko la kweli moyoni mwako. Mapito yako yasikufanye uache kuliishi katika Neno. Petro alimwambia Yesu kwa neno lako nitashusha nyavu. Liamini Neno. 

Maandiko mengine
Math 7:24 - 27, Yoshua 1:8, na  1Tim 4:15

MHUBIRI
SAMWEL ZAYUMBA 
KUTOKA TAG MWENGE - DSM

Jumapili, 21 Mei 2017

SAA YA TAABU YAKO INAPITA

SAA YA TAABU YAKO INAPITA
2WAFALME 4: 1 -7 
Tarehe 21.05.2017

Saa ya taabu inapofika huumiza, huteta majuto, huteta maswali mengi, huleta manung`uniko, huwa na uchungu, hukosesha amani moyoni, huondoa furaha nakadhalika. Kwa upande wa mtu wa Mungu saa ya taabu inapofika huweza kumwondoa katika uwepo wa Mungu.

Mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha kwa habari za watoto wake wawili  kutaka kuchukuliwa ili wawe watumwa. Huyu mama alifiwa na mmewe na hakuwa na mali nyingi za kukidhi haja maisha yake ya kila siku. Yumkini alikuwa na madeni mengi hata yakampelekea kushindwa kulipa. Hakika ilikuwa saa ya taabu yake. Lakini Mtumishi wa Mungu Elisha alipofika nyumbani kule mama, mama yule akamwambia habari za watoto wake kutaka kuchukuliwa kuwa watumwa. Elisha akamwambia wataka nikufanyie nini? Niambie una kitu gani nyumbani? Mama yule akajibu akasema mimi ni mjakazi wakosina kitu nyumbani ila chupa ya mafuta. Ndipo Elisha akamwambia akisema nenda ukatake vyombo huko nje kwa majirani zako wote vyombo vitupu wala usitake vichache. Kisha uingie ndani ukajifungie mlango wewe na wanao ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote. Mama yule akafanya hivyo ndipo vyombo vyote vikajaa mafuta. Biblia inatuambia vyombo vilipokuwa vimejaa Mtumishi Elisha akamwambia mama niletee tena chombo. Mama akajibu akisema hakuna tena chombo. Hivyo mama yule saa ya taabu yake ikawa mwisho kwani mafuta yale aliyauza na kulipa manedi ili watoto wake waliende utumwani

Ndugu saa ya taabu yako inapita tu. Kwa nini kufadhaika, kuhangaika na hata kuvunjika moyo kwa taabu yako unayoipita. Kumbuka saa ya taabu inapita tu. Yesu yupo alipigwa msalabani kwa ajili ya taabu yako. Usimwache Yesu kwa taabu yayo unayoipitia. Ayubu hakumwach aMungu kwa taabu yake aliyoipata. Mweleze Yesu taabu yako naye atakutokea. SAA YA TAABU INAPITA USIOOGOPE.

Mhubiri
Mchungaji. Mary Mneo

KUNA NGUVU KATIKA NENO LA MUNGU

UJUMBE: KUNA NGUVU KATIKA NENO LA MUNGU
LUKA 5: 4 -11
Tarehe 14.05.2017

Luka aliandika habari zake baada ya kufanya utafiti wa jambo analotaka kuliandikia kama taaluma yake ya utabibu ambapo inamtaka kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kutoa tiba kwa mgonjwa.  Luka aliandika habari za Yesu na Simoni Petro kuhusu kushusha nyavu hadi kilindini ili wakavue samaki. Maandiko yanatuambia kuwa wakati Yesu anakutana na akina Simoni Petro muda wa kuvua samaki ulikuwa umepita na walikwisha kuosha nyavu zao ili warudi nyumbani kwani kwa kazi ya usiku ule haikuwa na mafanikio kwa kuwa hawakupata samaki. Ndipo Yesu akawaambia shusheni nyavu zenu mpaka kilindini mkavue samaki. Simoni Petro akajibu Bwana tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha tusipate kitu lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Basi wakaenda mpaka kilindini wakashusha nyavu zao mara nyavu zao zikaanza kuzama kwa wingi wa samaki wakaamua kuwaita washirika wenzao ili wasaidiane kuchukua samaki. Wakapata samaki wengi sana.

Hebu tuone nguvu ya kuliamini Neno la Mungu
Simoni Petro aliposema kwa Neno lako nitazishusha nyavu kwani alitambua kuwa kazi yao ya usiku kucha haikuwa na mafanikio na wao mahitaji yao yalikuwa ni kupata kitoeo na matumizi mengi kwa familia. Walichoka sana kwa kazi hiyo ya usiku kucha lakini wakaamua kulitii Neno la Mungu na kulitendea kazi kwa kushusha nyavu kama Bwana alivyosema. Je mimi na wewe leo tunaweza kufanya hivyo. Mbona ujumbe unapokuja kwako unaona si wako ila wa mtu mwingine? Hatupokei kutoka kwa Bwana kwa kutoliamini Neno la Mungu.

Ipo nguvu katika kuliamini Neno la Mungu. Neno la Mungu huleta matokeo chanya katika maisha ya mwamini ukiliamini sawa sawa na Neno lake.


Mhubiri
Mchungaji Kiongozi: P. Mneo

KILELE CHA JUMA LA CMF: CHANGAMKA USIOOPE

Ujumbe: Changamka usiogope
Marko 6: 45 - 51

Yesu aliwalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani na kuanza safari ya kuvuka ng`mbo hata Bethsaida. Yesu akabaki na makutano kwa kitambo kidogo. Wanafunzi wakaanza safari yako kwenda Bethsaida. Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari na Yesu yu pekee yake katika nchi kavu akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kuvuta makasia kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho hata ilipopata zamu ya saa nne ya usiku Yesu akawendea akitembea juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona walidhani ni kivuli wakapiga yowe kwa kuwa wote walimwona wakafadhaika. Mara akasema nao akawaambia " Changamkeni ni mimi hapa msioogope". Akapanda chomboni upepo ukakoma.

Mpendwa hata kama unapita katika magumu ya namna gani usioogope Yesu yupo kwa ajili yako anakuona ukitaabika hivyo mwamini yeye naye atakutokea katika majaribu yako CHANGAMKA USIOGOPE

Mhubiri
Ndg Donalth Kweka
Mwenyekiti CMF

YESU NDIYE SULUHISHO LAKO

UJumbe: YESU NDIYE SULUHISHO LAKO
Maandiko: Luka 5:12 - 14
Tarehe 30.04.2017

Ukoma katika jamii ya Israel ilikuwa ni tatizo kubwa mno. Mtu mwenye ukoma ililazimika kutengwa  kama tunavyosoma maandiko Mambo ya Walawi 13 - 14.

Hata sasa dunia huwatenga watu wenye ukoma. Ukoma hushambulia mwili na hata mfumo wa fahamu. Kwa zama za Agano la Kale mtu mwenye ukoma alitengwa kwa muda fulani mpaka atakapotasika na baada ya kutakaswa atoe sadaka maalumu. Kuhani alihusika kumkagua mtu mwenye ukoma kama ametakasika au la. Mtu mwenye ukoma akichangamana na watu wasio na ukoma sheria iliwaruhusu kumwua mtu huyo kwa mawe. 

Siku moja mwenye ukoma alisikia habari za Yesu na akazimia moyoni mwake kwenda kwake ili aponywe na ukoma. Ugonjwa huo ulimtesa kwa siku nyingi akaanguka kifudifudi mbele za Yesu akisema " Bwana ukitaka waweza kunitakasa". Ndipo Yesu akaunyoosha mkono wake akisema nataka takasika. Mara mtu mwenye ukoma wake ukamwondokea. 

Imani ya mtu mwenye ukoma ilimfanya atakasike na akawa huru kuchangamana na watu wengine

Mtu wa Mungu ukoma ni dhambi ambayo hutufanya tufarakane na Mungu. Ni kitu gani kwako ambacho ni ukoma kinakufanya usipokee muujiza wako? Nenda mbele za Bwana umweleze mambo yako na akurehemu ndipo upokee haja ya moyto wako kama vile mtu yule aliyekuwa na ukoma alipomwendea Yesu na kuanguka kifudifudi.


Mhubiri
Mchungaji Jonas Charles Shebila
T.A.G Michungwani Muheza



Jumapili, 23 Aprili 2017

UMEJIANDAEJE KWA AJILI YA UNYAKUO

Mchungaji Kiongozi akitoa ujumbe

IBAADA YA TAREHE 23.04.2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI KIONGOZI PASCAL MNEO
MAANDIKO: Math 24: 15 - 26
UJUMBE: Umejiandaaje kwa ajili ya unyakuo.

Utangulizi:
Wanafunzi wa Yesu walitaka kufahamu mambo matatu kutoka kwa Yesu ambayo ni 
  1. Tuambie lini yatatukia hayo
  1. Dalili ya kuja kwako (Yesu Kristo)
  1. Mwisho wa dunia itakuwa lini

JUMATAU YA PASAKA 2017

IBAADA YA JUMATATU YA PASAKA TAREHE 17.04.2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI MARY MNEO
MAANDIKO: WAEBRANIA 2:3
UJUMBE: KUJALI.
Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii? Yesu aliicha  enzi yake na kuja dunia kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu yaani mimi na wewe. Si hivyo tu pia alikubali kuchukuwa mateso yetu. Yeye wala hakustahili kupata mateso yale aliyoyapata msalabani. Ni upendo wake kwa ajili yetu. Wakati mwingine hatujali huu wokovu ambao hupatikana mara moja tu. Tunaweza kufanya tunayoyataka kwa kutojali wokovu ambao Yesu alijitoa hata kuutoa uhai wake pale msalabani. Alisema Baba imekwisha pale kalivari. Unapotafakari upendo wa Yesu kwa ajili yetu hasa tunaposikia ujumbe huu wa tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii? Tuijali kazi kubwa ambayo Yesu aliifanya pale msalabani ili tupate kuwa haki ya Mungu.

KUNYAKULIWA KWA KANISA

IBAADA YA TAREHE 02.04.2017
MAANDIKO: Math 24: 36 - 44
Mhubiri: Mchungaji  
Ujumbe: Kunyakuliwa kwa kanisa


  Mathayo aliitwa na Bwana Yesu na kuambiwa "nifuate". Mathayo alimfuata Yesu bila ya kujiulizauliza. Hivyo Mathayo akawa miongoni mwa wale Thenashara ( wanafunzi 12).


Yesu alianza kueleza namna siku hiyo itakavyokuwa kwa kuanza na mfano wa Gharika wakati wa mtumishi wa Mungu Nuhu. Watu waliendelea kufanya shughuli zao na Nuhu hakuacha kuwaambia watu habari za mpango wa Mungu wa kugharikisha ulimwengu. Nuhu aliwaitwa watu waje watengeneze safina ili waokolewe lakini watu hawakujali na walimwona Nuhu kama mtu aliyechanganyikiwa. Kwenye gharika hiyo alipona Nuhu na familia yake tu.

Jumapili, 26 Machi 2017

IBAADA YA MEZA YA BWANA

IBAADA YA MEZA YA BWANA TAREHE 26.03.217
Ibaada hii imefanywa na Mchungaji Kiongozi P. Mneo

Maandiko 1Kor 11: 24 - 32

Matukio katika picha.


Mchungaji Kiongozi akitoa ujumbe wa Meza ya Bwana
Mchungaji Mary Mneo akiombea mkate


Mzee wa kanisa ndg Frida Kweka akiombea divai

Viongozi wakiwa tayari kuhudumu meza ya Bwana





JE UMEIMIMINA ROHO YAKO KWA NANI?

IBAADA YA TAREHE 26.3.217
MHUBIRI: Ndg VERONICA MALUWA
UJUMBE: Je umeimimina roho yako kwa nani?
Maandiko: 1Samwel 1: 9 - 20





1Samwel 1:15 ( ......... mimi sikunywa divai wala kileo ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana).

Utangulizi: 
Kumimina roho kwa Bwana ni ile hali ya kupeleka au kueleza haja ya moyo kwa Mungu kwa unyenyekevu mkuu. 

Palikuwa na mtu mmoja mcha Mungu aliyeitwa Elkana. Naye Elkana alikuwa na wake wawili mmoja aliitwa Hana na wa pili aliitwa Penina. Penina alikuwa na watoto lakini Hana hakuwa na mtoto kwa wakati ule kwa Mungu alimfunga tumbo lake kwa muda. Moyo wa Hana ulikuwa na huzuni kwa kukosa mtoto ndipo akaamua moyoni mwake kuimimimna roho yake kwa Bwana. Mungu akasikia haja ya moyo wake hatimaye akapata mtoto wa kiume akamwita jina Samwel.

Ujumbe 
Katika maisha yetu ya kila siku yapo mahitaji mbalimbali na mengine ni magumu kwetu lakini ukiimimina roho yako kwa Bwana naye atafanya kwa ajili yako. Yeye ni mwaminifu ukitembelea pamoja naye kama Hana alivyofanya.

Faida ya kuimimina roho yako kwa Bwana
  1. Bwana atakulinda (Mdo 16: 25) 
  2. Bwana atakuinua  (Mwanzo 41: 45)
  3. Kwake yeye ni kimbilio na nguvu (Zab 46:1)
Hitimisho
Inawezekana mpendwa hupokei haja ya moyo wako kwa kuwa hujaimimina roho yako kwa Bwana. Mimina haja ya moyo wako kwa Bwana naye atakutokea. Kwa Mungu wetu hakuna jambo asiloliweza tazama mfano wa Shadrack, Meshack na Abedinego katika tanuri la moto Mungu alichowafanyia. Tusikate tamaa wala kumtenda Mungu dhambi. 

IBAADA YA KUWAWEKA WAKFU WATOTO

IBAADA YA KUWAWEKA WAKFU WATOTO TAREHE 26.03.2017


Matukio katika picha. Tazama picha hapa chini









Jumapili, 19 Machi 2017

NANYI MWANINENA KUWA MIMI NI NANI?

IBADA YA TAREHE 19.03.2017
MHUBIRI: NDG DICKSON A. MFIKWA
UJUMBE: Nanyi mwaninena kuwa mimi ni nani?

Maandiko: Math 16: 13 - 16













Utangulizi
Kitabu cha kwanza kabisa katika Agano Jipya ni kitabu cha Injili ya Mathayo. Kitabu hiki kinasadikiwa kiliandikwa na Mathayo Mwenyewe kwenye mwaka 65 - 70 BK. Lengo la kuandikwa  kwa kitabu hiki ilikuwa kuthibitisha kuwa Yesu Kristo ni Masihi wao wa kweli.

Somo lenyewe.
Maana ya Masihi au Masiya:
   Mtu anayeaminiwa na wakristo kuwa ni Mwana wa Mungu aliyezaliwa kuwaokoa watu dhidi ya dhambi, Mkombozi, Yesu Kristo (kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu).

Siku moja Yesu akaamua kuwauliza wanafunzi wake kuhusu maisha yake akitaka kufahamu hasa watu wanamnenaje kuhusu yeye mwenyewe. Kwa maana nyingine aliamua kufanya tathmini ya maisha yake. Kupitia maisha au huduma ya Yesu Kristo aliyokuwa akifanya watu walimnena kuwa yeye huhenda ni Yohana Mbatizaji, Elia, Yeremia au miongoni mwa Manabii. Hivyo ndivyo wanafunzi walivyojibu swali ambalo Yesu Kristo alilouliza. Yesu hakuishia hapo akawauliza tena wanafunzi nanyi mwaninena kama mimi ni nani? Ndipo Petro akajibu kuwa wewe ni Mwana wa Mungu aliye hai.

Zipo sababu zizowafanya watu wengine waseme kuwa Yesu Kristo ni Yohana Mbatizaji, Elia, Yeremia au ni miongoni mwa Manabii. Kati ya sababu hizo ni nguvu alizokuwa nazo Yesu Kristo katika huduma yake kama vile vipofu waliona, viwete walitembea, wenye ukoma walitakasika, wafu walifufuka, wenye mapepo walitolewa, wagonjwa walipata nguvu nakadhalika.

Maisha mkristo wa leo
Nasi katika maisha tunayoyaishi hatuna budi kujifanyia tathmini kama Bwana wetu Yesu Kristo alipoamua kujitathmini juu ya maisha yake kwa watu waliokuwa wakimzunguka pamoja na wanafunzi wake. Leo maisha yetu yamezuia nguvu za Mungu kutendeka ndani ya kanisa kwa sababu ya ushuhuda wa maisha yetu kwa watu waliopo ndani na nje ya kanisa. Inatupasa kufanya tathmini ya maisha yetu ili tuweze kubalika na kumlingana Bwana wetu Yesu Kristo. Tuone ni wapi tunakosea na kutubu kama Isaya alivyofanya (Isaya 6:5). Matendo, Maneno na mawazo yawe safi mbele za Mungu.

Madhara ya kutenda dhambi

  1. Utasababisha hata asiye na hatia kuangamia kwa ajili yako. (Yoshua 7: 1, 5, 20, 24)
  2. Nguvu za Mungu hazitendi kazi ndani yetu

Hitimisho. 
Mpendwa tukitaka nguvu za Mungu zitende kazi ndani yetu na watu wengine waokolewe hatuna budi kuacha kutenda dhambi na kuishi maisha yenye ushuhuda mzuri mbele za Mungu.




Jumapili, 12 Machi 2017

MUNGU HUSIMAMA NA MWENYE HAKI

IBADA YA TAREHE 12.03.2017

MHUBIRI: MCHUNGAJI MARY MNEO
UJUMBE: Mungu husimama na mwenye haki


Mchungaji Mary Mneo akihubiri
Mambo tunayojifunza katika Mwan 6: 1 - 13 ni kama ifuatavyo:-

  1. Mtazamo wa wana wa Mungu haukuwa kama Mungu alivyokusudia.
  2. Mungu anaweka hisia zake wazi juu ya kutoshindana na mwanadamu
  3. Mungu anayaona mawazo ya mwanadamu kuwa ni mabaya siku zote.
  4. Nuhu anapata neema machoni pa Mungu.
Kilichomfanya Nuhu kupata neema machoni pa Mungu katika dunia iliyojaa dhuluma ni kutembea pamoja na Mungu.

Hitimisho: Hata sasa mtu wa Mungu fanya maamuzi ya kutembea pamoja na Mungu. Haijalishi tupo kwenye dunia ya namna gani bado tunaweza kupata neema machoni pa Mungu kama ilivyokuwa kwa Nuhu.


IBADA YA KUWAWEKA WATOTO WAKFU KWA MUNGU

Mchungaji na wazazi wenye watoto wa kuwekwa wakfu kwa Mungu


Mchungaji akipoke mtoto kutoka kwa mzazi

Mchungaji Kiongozi akiombea mtoto



 Hizi ni baadhi ya picha katika matukio ya ibada ya kuwaweka watoto wkfu kwa Mungu.

Jumapili, 5 Machi 2017

KILELE CHA JUMA LA WWK 2017


Tarehe 5.3.2017
KILELE CHA JUMA LA WWK
MHUBIRI: M/KITI NDG FRIDA KWEKA

Mwenyekiti WWK akitoa ujumbe


 UJUMBE: JE WATAKA KUPONA?
Ebr 2:3, Yoh 5:24, Fil 3:7 - 8 na Yuda 1:3

Ili tuweze kupona hatuna budi kufanya yafuatayo


      1. Kufanya mambo ya Mungu kwanza halafu yetu baadaye.
      2. Kuvaa silaha za Mungu. (Efe 6: 10 - 18).
      3. Kujitambua











MATUKIO KATIKA PICHA

Viongozi wa WWK wakiwa mbele ya Madhabahu

WWK wakiimba wimbo wao

Hawa ni WWK wakiongoza Ibada ya sifa na kuabudu


Mchungaji na Mama Mchungaji

Familia ya Mchungaji


Mchungaji na mama Mchungaji wakipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa WWK


Jumapili, 26 Februari 2017

KUISHI MAISHA YA USHINDI

Tarehe 26.2.2017Somo: Kuishi maisha ya ushindi

Efeso 6: 12

Adui yetu anajua uzuri wa Mbinguni hivyo anashindana nasi ili tusiende mbinguni. Shetani hushambulia maisha ya mwamini kama tunavyosoma Ayubu 1: 6 - 12

Kwa hiyo ndugu maliza maishi ya ushindi kwa kufanya yafuatayo:-

  • Kuwa msomaji wa Neno la Mungu
  • Kuwa mwombaji (Yoshua 10: 12)
  • Kuwa na imani thabiti
  • Kuwa na moyo wa sifa
  • Kuwa na shukrani
  • Kuwa na roho ya kusamehe

HITAJI LANGU BAADA YA KUOKOKA

Tarehe  19.2.2017

Somo: Hitaji langu baada ya kuokoka:

Yafuatayo ni mahitaji ya lazima baada ya mtu kuokoka

  1.  Ujae Roho Mtakatifu
  2. Ubatizo wa maji mengi
  3. Kudumu katika mafundisho ya Neno la Mungu (1Petro 2:2)
  4. Ushirika wa Meza ya Bwana (1Kor 11: 23 - 26)
  5. Ushirka na wengine waliookoka
Maadui wa mtu aliyeokoka
  1. Ulimwengu/Dunia (1Yohana 2: 16 - 17)
  2. Mwili (Rumi 8: 1 - 13, Galatia 5: 13 - 17, Yak 4: 1 - 10)
  3. Nafsi (Mwa 6: 1 - 6)
  4. Mazingira (Mwa 34: 11 - 12)
Wajibu wa mtu aliyeokoka
  1. Kuishi maisha Matakatifu
  2. Kumtafuta Roho Mtakatifu
  3. Kumcha Mungu katika Roho kwa viwango vya juu
  4. Kumjua Mungu wa Biblia
  5. Kumjua Yesu
  6. Kuwa mwakili wa siri za mbinguni
  7. Kuwa na chumvi za dunia
  8. Kuwa nuru ya Ulimwengu
  9. Kuwa taa ya Ulimwengu
  10. Kuwa barua
  11. Kuwa mhubiri wa Injili
  12. Kuwa mwombaji
  13. Kuwa msafiri wa kwenda mbinguni


Jumapili, 1 Januari 2017

UJUMBE WA MWAKA MPYA 2017

SOMO: UMWANGALIE BWANA

Isaya 45:22 " Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia, maana mimi ni Mungu, hapana mwingine". 

Mwaka 2017 Bwana anasema niangaleni mimi. Ili mwaka huu ufanikiwe, ubarikiwe au unapopita kwenye magumu yoyote umwangalie yeye aliye juu (MUNGU). 

Inawezekana mwaka 2016 ulimwangalia mwanadamu lakini mwaka huu 2017 geuza macho yako umwangalie Mungu maana hakuna mwingine ila yeye pekee yake.